![]() |
Ufugaji wa Samaki Ndani ya Vizimba (Cage Farming) |
Uvuvi wa Kisasa na Ufugaji wa Samaki Wakua Kiuchumi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imekuwa kinara wa mapinduzi katika sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki. Kupitia mikopo nafuu na ya kimkakati, TADB imefungua milango ya uchumi kwa wavuvi wadogo, vijana na wakulima wa maji nchini.
Uvuvi wa Kisasa kwa Mashua za Kisasa
Kwa kutoa zaidi ya TZS bilioni 14.23, TADB imefadhili ununuzi wa boti 190, na kuwawezesha wavuvi wadogo 3,329 katika mikoa 16 kubadili maisha yao kutoka uvuvi wa kujikimu hadi kibiashara. Mafanikio haya yamechochea:
-
Thamani ya mazao kuongezeka kupitia huduma za baridi na uchakataji wa samaki.
-
Ajira mpya kupitia wauzaji wa vifaa, mafundi na wauza samaki.
-
Wavuvi wengi kuingia rasmi katika mfumo wa kifedha—wengi wao wakiwa hawakuwa na akaunti awali.
Ufugaji wa Samaki Ndani ya Vizimba (Cage Farming)
-
Ujenzi wa vizimba 337.
-
Wakulima wa maji 1,631 kufaidika, ikiwemo vijana 1,223.
Mafanikio haya yameleta mabadiliko ya kweli:
-
Samaki zaidi ya tani 2,651.8 zimevunwa, na kuchangia TZS bilioni 2 kwenye uchumi wa mikoa.
-
Familia zimeanza kupata kipato cha uhakika na maisha bora.
-
Vikundi 25 vililipa mikopo yao ya awali na kupewa tena mikopo kwa awamu ya pili.
-
Vijana waliowezeshwa ni asilimia 75 ya walionufaika na ufugaji huu wa kisasa.
-
💸 TZS Bilioni 8.36 – Fedha zilizotolewa kwa ajili ya ufugaji wa samaki Kanda ya Ziwa
-
🛖 Vizimba 337 – Vimejengwa kwa wakulima wa maji
-
🧑🏽🌾 Vijana 1,223 – Wamepata ajira kupitia ufugaji wa samaki